Loading...
fr


Baadhi ya wakulima waliohudhuria kwenye mkutano huo
Image caption Baadhi ya wakulima waliohudhuria kwenye mkutano huo

Wakulima nchini Tanzania wameonywa kujiepusha na matumizi ya mbegu za kisasa kwa madai kwamba zinawafanya wakulima wadogo kuwa tegemezi kwa makampuni makubwa ya mbegu.

Wito huo umetolewa na Prof. Issa Shivji ambae ni mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere katika mkutano wa 22 wa kila mwaka wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima nchini Tanzania.

Mbali na hayo, prof. Shivji pia aliwatahadharisha wakulima kuilinda ardhi yao na kuacha kuichukulia mikopo.

Zaidi ya wanachama 250 kutoka mikoa mbali mbali nchini Tanzania wamehudhuria mkutano huo wa siku mbili uliofanyika nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Viongozi mbalimbali walihudhuria mkutano huo wakiwemo wakuu wa wilaya za Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Mkoa na wataalamu waliobobea katika masuala mbalimbali kama vile prof. Issa Shivji na Joseph Butiku kutoka Mfuko wa Mwalimu Nyerere.

Image caption Joseph Butiku (kulia) ni miongoni mwa watu wenye mchango mkubwa kwenye sekta ya kilimo Tanzania

Akiainisha changamoto mbalimbali zinazomkabili mkulima, Veronica Sophu ambae ni mwenyekiti wa mtandao wa wakulima wadogo wadogo Tanzania MVIWATA, amesema katika sera ya viwanda hakuna mpango mkakati wa kuwafanya wakulima kuingia kwenye mpango wa viwanda, hivyo kuitaka serikali kuandaa mpango ambao utawashirikisha wakulima katika mpango wa viwanda.

"Tunapenda mpango uandaliwe, tushirikishwe, tujikite ni sehemu ya kuelekea Tanzania ya viwanda.Unapozungumzia Tanzania ya viwanda halafu ukamuacha nyuma mkulima mdogo, mwisho wa siku huwezi kufikia uchumi wa kati."

Nae waziri wa kilimo Dkt. Charles Tizeba ambae ndie aliyekuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, akijibu baadhi ya hoja zilizoibuka, amesema suala la uongezaji thamani kwa bidhaa za kilimo lazima litiliwe mkazo kupitia viwanda.

"Tunajua kuwa kuna mazingira ambayo sio wezeshi kwa kilimo ikiwa ni pamoja na kodi, sheria, miongozo, makatazo, yote ni mambo ambayo yanafanya kilimo kisiende kwa kasi, au yanatengeza mazingira ambayo sio rafiki kwa wazalishaji wa bidhaa za kilimo.Haya ni mambo ambayo tunaona kama serikali, tuyafanyie kazi kwa umakini mkubwa ili kuwajengea mazingira wakulima kuweza kuongeza uzalishaji," alisema waziri Tizeba.

Image caption Waziri wa kilimo Tanzania Charles Tizeba mwenye suti ameelezea mikakati ya serikali katika kuondoa changamoto za wakulima

Jovita Banyeza ambae ni mkulima mdogo kutoka Mkoani Kagera, amesema changamoto iliyopo ni serikali kutomwangalia mkulima wakati wa kulima, lakini wakati wa kuvuna ndipo inapoingia kati.

"Tunajua serikali imeondoa baadhi ya tozo, lakini sisi wakulima wadogo wa Kagera hatujui ni tozo gani hizo, hivyo tunaiomba serikali ituelimishe kuhusu tozo zilizoondolewa," amesema Jovita.

Siku ya kwanza ya mkutano huo umehusisha warsha iliyojadili haki za wakulima.

Pamoja na hayo pia, kumekuwa na uchaguzi wa viongozi wa mtandao.

Le Mur

Aucun commentaire
Tu dois te connecter pour commenter

Votez !

Ta note :
Total : (0 votes)

Actus

Publié il y a moins d'une minute
Publié il y a moins d'une minute
Publié il y a moins d'une minute
Publié il y a moins d'une minute
Publié il y a moins d'une minute

African FM

RFI Afrique

Radio Okapi